Tunasaidia biashara zako kukua mtandaoni, kupata wateja na kuongeza mauzo kupitia usimamizi wa mitandao ya kijamii na Meta Ads
Tunasaidia biashara zako kujenga uwepo imara mtandaoni kwa kusimamia kikamilifu akaunti zako za mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Instagram na TikTok. Huduma zetu zinahusisha kupanga na kuandaa maudhui (content creation), kuhariri na kuchapisha posti na reels kwa mpangilio unaolenga kuvutia na kuhusisha wateja wako.
Pia tunasimamia matangazo ya kulipia (Meta Ads) kwa ufanisi kwa kuchagua audience sahihi, kudhibiti bajeti, na kuboresha matangazo kulingana na matokeo halisi. Tunafuatilia utendaji wa matangazo na akaunti zako kwa karibu na kukuletea ripoti za mara kwa mara ili ujue maendeleo ya biashara yako mtandaoni.
Lengo letu ni kukuondolea stress ya kusimamia mitandao ya kijamii, huku tukihakikisha biashara yako inapata mwonekano mkubwa, wateja wengi na ongezeko la mauzo kwa njia ya kitaalamu na yenye matokeo.